Nukuu za Mwl. Nyerere zinazoishi

HomeKimataifa

Nukuu za Mwl. Nyerere zinazoishi

Aprili 13 kila mwaka ni siku ambayo watanzania wanaadhimisha kuzaliwa kwa Hayati baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kiongozi aliyefanikisha uhuru wa Tanganyika na kujulikana kama mpenda amani aliyetaka kuwaunganisha sio tu Watanzania bali Waafrika. 

ClickHabari tumekuandalia baadhi ya Nukuu za Mwalimu ambazo aliwahi kuzisema na bado zinaishi katika maisha yetu ya kila siku.

  1. Hakuna taifa lenye haki ya kufanya maamuzi kwa ajili ua taifa jingine, hakuna watu kwa ajili ya watu wengine.
  2. Elimu sio njia ya kuepuka umaskini, ni njia ya kupigana nao.
  3. Demokrasia sio chupa ya Coca-cola ambayo unaweza kuiagiza. Demokrasia inapaswa kuendelezwa kulingana na nchi yenyewe.
  4. Itakuwa yote ni makosa, na si jambo la muhimu,kuhusi kuwa lazima tusubiri hadi viongozi wafe ndio tuanze kuwakosoa.
  5. Wengine humwona mwenzao anafanya kosa.Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya.Lakini hawanyamazi kimya kabisa! Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri siri.
  6. Watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu, wala hawana haja kujifunza zaidi.Hii ni tabia mbaya ambayo huzuia kabisa maendeleo.
  7. Hatuwezi kuwa na matumaini ya kutatua matatizo yetu kwa kujifanya kuwa hayapo.
  8. Tunataka kuona vijana jeuri katika Taifa hili na wenye kujiamini na sio waoga akina ” ndiyo bwana mkubwa”. Tunataka kuona vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya kidhalimu isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa. 
  9. Nawaambieni na msikilize kwa makini: UTII ukizidi sana unakuwa WOGA. Mara zote utii huzaa unafiki na kujipendekeza. Sasa nyinyi watumishi wa umma kwa wingi wenu kama mmeshindwa kupiga kura kuondoa viongozi dhalimu, bora mfe tu.

10. Ukweli una tabia moja nzuri sana.Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki.Kwake watu wote ni sawa.

error: Content is protected !!