Kwa wale wapenzi wa fasheni na bidhaa zenye majina watakuwa wameisikia sana Balenciaga kampuni ambayo inatengeneza bidhaa za fasheni za kisasa na za gharama sana duniani, nao wamekuja na raba ambayo muonekano wake na bei havilandani.
Balenciaga wamekuja na raba zenye muonekano wa raba ilizochakaa na hazifai kuvaliwa tena “Destroyed sneakers” kwa $1,850 ~ TZS 4.3m. Huku mitandao ikiendelea kujadili kiatu hicho Balenciaga imewakumbusha wadau wao kuwa raba hizo hazipo nyingi na zitaisha sokoni mapema sana kwani zipo jozi 100 tu.
Jozi hizo 100 ni ya zile zilizoharibika zaidi “extra destroyed” huku zilizochanika kidogo zikienda kwa bei ya kati ya $495 – $625 sawa na shilingi milioni 1.2 hadi milioni na nusu.
Je! Upo tayari kutumia kununua jozi ya raba hizi?