Bei ya petroli Marekani inazidi kupaa

HomeKimataifa

Bei ya petroli Marekani inazidi kupaa

Jumuiya ya wenye magari ya Marekani imesema mfumuko wa bei ya mafuta nchini humo umeizidi kupaa huku galoni moja yenye uzito wa lita 3.78 iliuzwa kwa dola 4.374.

Bei ya petroli imepanda kwa asilimia 9.4 nchini Marekani na hii imepelekea nchi hiyo kuanza kushirikiana na baadhi ya nchi duniani kuongeza idadi ya usambazaji mafuta katika soko la dunia, ili kudhibiti bei.

Hali ya upatikanaji wa mafuta sio nzuri baada ya kutokea vita vya Ukraine na hatua zilizochukuliwa na nchi za magharibi za kuiwekea vikwazao vikali Urusi.

Aidha, taarifa za kuaminika kutoka vyanzo vitatu zinadai Machi, mwaka huu viongozi wa Marekani waliiomba Brazili iongoze kiwango cha mafuta yake katika soko la dunia lakini nchi hiyo ilikataa ombi hilo.

error: Content is protected !!