Atoroka nyumbani kisa kufeli mitihani

HomeKitaifa

Atoroka nyumbani kisa kufeli mitihani

Dorice Venance (16) mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Migamboni, anadaiwa kutoroka nyumbani kwao Tabata Segerea tangu JUni 4, mwaka huu kwa madai ya kufeli kwenye mitihani yake.

Baba mkubwa wa manafunzi huyo, Charles Kenyela alisema, alimtoa Dorice nyumbani kwao Mwanza baada ya kumaliza elimu ya msingi na kumhamishia Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na masomo ya sekondari ili kumpa msaada wa kielimu.

“Hivi karibuni alishawahi kuniambia kuwa anaomba nimrudishe nyumbani kwao Mwanza kwa sababu anahisi kuwa anapoteza muda kutokaa na kufeli mitihani yake kadiri siku zinavyokwenda,” alisema Kenyela.

Hata hivyo, alisema alimtia moyo na kumshauri aongeze bidii kwa sababu elimu ya kijijini aliposoma msingi ni tofauti na mjini, lakini Jumatano ya wiki iliyopita mtoto huyo akitoroka saa tano usiku akiwa amevaa shtai la rangi ya kahawia na suruali ya kulalia ya bluu.

“Tuligundua kuwa ametoroka baada ya kukuta funguo zikining’ia mlangoni na tulipotazama kwenye kamera za CCTV tukamuona alivyokuwa anatoroka. Mpaka sasa kwao Mwanza hajafika na wala hapa nyumbani hayupo,” alisema Kenyela.

Aidha, tayari taarifa walipeleka Kituo cha Polisi Tabta na kupewa RB Na. TBT/RB/2635/2022 kwa yeyote atakayemuona atoe taarifa kwenye kituo hicho au kupiga simu namba 0743608494. 

Newer Post
Older Post
error: Content is protected !!