10 mbaroni kifo cha askari Loliondo

HomeKitaifa

10 mbaroni kifo cha askari Loliondo

Jeshi la Polisi limewakamata watu 10 kwa tuhuma za kuhusika na vurugu zilizojitokeza wakati wa uwekaji wa mipaka kwenye eneo la pori tengefu la Loliondo, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Liberatus Sabas, alisema watu wao wamekamatwa katika operesheni inayoendelea kufanywa na jeshi hilo.

Katika vurugu hizo askari namba G4200 mwenye cheo cha Koplo, Garlus Mwita Galus ambaye alikuwa akifanya kazi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma aliuawa kwa kuchomwa mshale.

“Tumewakamata watu 10 na hii operesheni itakuwa endelevu hadi tuhakikishe wote waliohusika wanatiwa mbaroni,”

“Yeyote aliyeshiriki kupanga, kuratibu na mwisho kutekeleza tukio hili hatakuwa salama, tutamsaka usiku na mchana hatimaye sheria itachukua mkondo wake,”alisema Kamanda Sabas.

 

error: Content is protected !!