TRA yatoa ufafanuzi tuhuma za Mama Kibonge

HomeKitaifa

TRA yatoa ufafanuzi tuhuma za Mama Kibonge

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi kwa umma kuhusu tuhuma zilizokuwa zikitolewa kwenye mtandao wa ‘twitter’ kuwa ilikua inakusanya kodi kwa kutumia mabavu eneo la Kariakoo juzi muda wa saa saba usiku kwa mfanyabiashara Bi. Salome Mgaya maarufu kama Mama Kibonge.

TRA imesema ilikua ikifuatilia tuhuma zilizokuwa zikitolewa dhidi ya mfanyabiashara huyo za uingizaji wa bidhaa za vitenge nchini kwa njia za magendo ambapo hivi karibuni uchunguzi ulibaini kuwa, kulikuwa na makasha mawili yenye mizigo ambayo nyaraka zake zilionesha kuwa bidhaa zilikuwa ndani yake zilikuwa ni mashuka zikielekea Chitipa Mzuzu nchini Malawi.

Taarifa kutoka TRA zinasema bidhaa hiz hazikuwa mashuka kama nyaraka zilivyoonesha bali zilikuwa ni vitenge vinavyotarajiwa kuingizwa nchini pasipo kulipiwa kodi (dumping) na zilihisishwa na mfanyabiashara huyo.

Shehena hizo baada ya kutoka Bandari ya Dar es Salaam usiku saa 7 na dakika 56, kasha moja lililokuwa limepakiwa kwenye Lori namba T680 AGN/ T439 AEB linalimilikiwa na Ndugu Yusuph Suleiman Ramadhan lilipofika maeneo ya Tabata Matumbi, lilichepuka kuingia kwenye Maghala ya Bidhaa ambapo Kikosi cha Kuzuia Magendo kwa kushirikiana na Askari Polisi walikuta lori hilo limeanza kushusha shehena hiyo ambayo ilithibitika kuwa ni Marobota 290 ya vitenge ambavyo vilihifadhiwa Kariakoo kwa mfanyabiashara huyo.

error: Content is protected !!