Mwendeshaji mpya wa DART apatikana

HomeKitaifa

Mwendeshaji mpya wa DART apatikana

Serikali inatarajia kusaini mkataba na mwendeshaji mpya wa Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Haraka jijini Dar es Salaam (DART) kutoka Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE).

Haya yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Jerry Silaa baada ya kuchambua taarifa ya utendaji kazi ya Wakala wa DART na kusema mkataba huo utasainiwa mwezi ujao.

Silaa alisema hivi sasa mradi huo umekuwa ukiendeshwa kwa kipindi cha mpito na kampuni ya Usafirishaji jijini Dar es Salaam (UDART).

“Wametuahidi kuwa mwanzoni mwa Septemba watasaini mkataba wa makubaliano na kampuni kubwa kutoka nchi za UAE. Kikubwa kamati imeendelea kuwapongeza utakumbuka UDART ilipoanza ilikuwa na tiketi za kielektroniki baadaye ikaingia katika tiketi za mkono,” alisema.

error: Content is protected !!