Mrithi wa TICTS apatikana

HomeKitaifa

Mrithi wa TICTS apatikana

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imepata mtoa huduma w amuda, Kampuni ya Adani Zone Limited (APSEZ) ya nchini India atakayefanya kazi ya kuondoa makasha na mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.

Jukumu hilo awali lilikuwa likifanywa na kampuni binafsi ya kimataifa ya kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) ambayo mkataba baina yake na TPA ulidumu kwa miaka 22.

Hatua hiyo inakuja baada ya mkataba wa miaka mitano uliosainiwa Julai 6,2017 kufikia ukomo Sptemba 30, mwaka jana, licha ya kuwepo kipengele cha kuuhuisha menejimenti ya TPA ilikataa.

Jana, ikiwa ni siku ya Kwanza Bandari ya Dar es Salaam , kuhudumiwa na mamlaka hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TPA , Plasduce Mbossa alisema,”leo (jana) tumeanza kusimamia kitengo sisi wenyewe na afanyakazi wote wa TICTS tumewachukua sisi.”

Mbossa alisema taratibu zote zinabakia vilevile kama zilivyokuwa mwanzo.

“Hakuna kinachobadilika, lengo tunalokusudia ni kuongeza ufanisi wa bandari yetu ili kuwa na bandari inayotoa huduma kwa viwango vya juu ziaid,” alisema Mbossa.

error: Content is protected !!