Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo endelevu na pia kusonga mbele.
Dkt. Kikwete ametoa pongezi hizo mbele ya wageni waalikwa waliohudhuria na kushiriki ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Demokrasia Barani Afrika unaowahusisha Viongozi Wakuu Wastaafu wa Nchi mbalimbali uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha.
“Ni jambo linalogusa moyo kufahamu kwamba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yako yenye heshima imeendelea kusimama imara na kusaidia kusonga mbele. Hamlindi tu mafanikio yaliyopatikana hadi sasa, bali pia mnajitahidi na kujitolea kwa dhati kuendeleza nchi kwenye mafanikio makubwa zaidi.
“Hongera kwa uongozi wako na tafadhali endeleeni na kazi nzuri, kama vile kauli mbiu yako ya “KAZI IENDELEE.”- alisema Dk. Kikwete.
Aidha, Dk. Kikwete ameshauri viongozi wa Afrika kuangalia na kuelewa kikamilifu hali ya sasa ilivyo barani na kuzitafakari changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo kwa muda mrefu ili waweze kupata maendeleo ya kisiasa na kiuchumi.
Nina mtazamo kwamba ili mtu aweze kuelewa kikamilifu hali ya sasa barani Afrika, ni vyema kutafakari changamoto ambazo tumekuwa tukipambana nazo katika uwanja wa maendeleo ya kisiasa na kiuchumi.