Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2022 inaeleza kwamba chombo cha habari kinachotumika zaidi ni redio ambapo 32% ni wanawake na 52% ni wanaume wenye umri wa miaka 15-49 wanasikiliza redio angalau mara moja kwa wiki.
Kwa upande wa televisheni, 30% ya wanawake na 47% ya wanaume wanatazama angalau mara moja kwa wiki, huku 6% ya wanawake na 21% ya wanaume wanasoma magazeti kila wiki.
Aidha, ripoti inaeleza 54% ya wanawake na 34% ya wanaume hawapati huduma hizi tatu za habari angalau mara moja kwa wiki.