Wasiomaliza ujenzi wa shule za sekondari kukiona cha moto

HomeKitaifa

Wasiomaliza ujenzi wa shule za sekondari kukiona cha moto

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa onyo kwa wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha kwamba ujenzi wa miundombinu yote katika shule za sekondari unakamilika kabla ya tarehe 30 Novemba 2023.

Amesema hayo leo Novemba 10, 2023 alipokua akihutubia bunge wakati wa kuahirisha vikao vya bunge jijini Dodoma.

“Serikali itachukua hatua kali kwa wote wataoshindwa kukamilisha ujenzi wa miundombinu katika Shule za Sekondari. Wakuu wa Mikoa fanyeni ufuatiliaji, Serikali imeshapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi katika Halmashauri zote nchini hivyo hakuna sababu wala visingizio vya kutokamilisha ujenzi kwa wakati.” alisema Waziri Majaliwa.

Aidha, jumla ya wanafunzi 1,206,995 sawa na 86.4% ya wanafunzi 1,397,370 waliosajiliwa kufanya mtihani na kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2023 wanatarajiwa kujiunga na Elimu ya Sekondari Januari,2024.

error: Content is protected !!