Tumia mbinu hizi ili bando la intaneti lisiishe haraka kwenye simu yako

HomeMakala

Tumia mbinu hizi ili bando la intaneti lisiishe haraka kwenye simu yako

Andiko hili fupi la kiteknolojia linakupa mbinu muhimu za kuhakikisha kwamba bando katika simu yako haliishi haraka ili uweze kufanya matumizi yako ya muhimu kwa raha. Kwa watumiaji wa Android
  1. Jiunge na Wi-Fi kila unapopata nafasi ya kufanya hivyo
Hii unaweza kuiita dezo lakini ni njia nzuri ya kuhakikisha bando ambalo umenunua kwenye simu yako linadumu. Hapa hakikisha kila sehemu unapokuta “Wi-Fi” ambayo una ruhusa ya kuitumia unazima data na kuitumia kuperuzi mtandao. Hii mbinu ni msaada mkubwa hasa kama unatumia kitu kinachokula bando kwa haraka kama ku-update simu au kutazama video mubashara (live streaming).
  1. Jenga tabia ya kutumia huduma za “streaming” kwa kiasi
Kama una programu/app unatumia ku-stream video au muziki hata kupakua na kupakia picha/video basi elewa hizo app lazima zitakuwa na matumizi makubwa ya bando. Wataalamu wanasema apps kama hizo ni bora ukatumia kwenye kompyuta badala ya kwenye simu ili kupunguza matumizi makubwa ya bando au utumie wakati una connection ya “Wi-Fi” kama mbinu namba moja inavyosema. 3. Badili “settings” za matumizi ya data kwa baadhi ya apps Kupunguza matumizi ya data kwa baadhi ya apps kutasaidia bando lako kutoisha mapema. Kuna baadhi ya apps hata kama hutumii muda huo huwa zinaendelea kula bando. Kwenye settings apps kama hizi inabidi ubadilishe na kuziruhusu kutumia bando pale tu unapozihitaji na sio muda wote. Ili kufanya hivyo fuata hatua zifuatazo kwenye Android yako:
  • Fungua setting
  • Nenda kwenye Apps
  • Bofya app unayotaka kupunguza matumizi yake ya data
  • Bofya mobile data
  • Kama sehemu ya matumizi ya data hata kama hutumii app hiyo iko on utaona hii sehemu ya mobile data ina alama nyeupe na bluu. Ili kuzima ibpfye iwe rangi nyeupe pekee.
Kwa watumiaji wa iPhone
  • Zima automatic updates zisiwe zinafanyika kwa bando la simu bali tu pale unapokuwa sehemu yenye “wi-fi”. Fuata hatua hizi: Nenda katika Settings > iTunes & App Stores > Turn Off Use Cellular / Mobile Data.
  • Zima apps zisiwe zinafanya Background Refresh. Hii maana yake apps zitaji-update pale tu unapotaka wewe. Fuata hatua hizi: Settings > General > Background App Refresh > Turn Off au changua baadhi ya apps
  • Zima iCloud isifanye kazi wakati unatumia bando la simu. Ifanye tu pale unapokuwa kwenye “Wi-Fi”. Fuata hatua hizi: Settings > Cellular / Mobile Data > Turn Off iCloud Drive
  • Zima baadhi ya apps ambazo hutaki zitumie bando bali “Wi-Fi” pekee. Fuata hatua hizi: Settings > Cellular > Chagua apps ambazo hutaki zitumie bando la simu (cellular data).
error: Content is protected !!