Rais wa Kenya, Mhe. William Ruto, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunda Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na tume hiyo.
Rais Ruto amesema kuundwa kwa tume hiyo, iliyoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman, ni ishara kuwa mataifa ya Afrika yana uwezo wa kutatua changamoto zao kwa kutumia mifumo ya ndani.
Kwa upande wake, Rais Ruto amesema kuwa Kenya pamoja na ukanda mzima wa Afrika Mashariki unaunga mkono juhudi zilizofanywa na Tanzania katika kulinda na kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumishwa.
Rais Ruto yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, ambapo anatarajiwa kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho, tarehe 05.


