Dkt. Gwajima atoa maagizo mazito MSD, NHIF

HomeUncategorized

Dkt. Gwajima atoa maagizo mazito MSD, NHIF

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amewataka watendaji wanaohusika na mnyororo wa ugavi wa dawa na vifaa tiba kuwa wazalendo, wawajibikaji na wawazi ili kudhibiti upotevu wa dawa.

Amesema ili kuboresha huduma za afya na upatikanaji wa dawa nchini, serikali imejenga viwanda vipya 18 vinavyozalisha dawa na vifaa tiba ambapo lengo la serikali hadi kufikia mwaka 2030 kuwa na uwezo wa kuzalisha dawa kwa asilimia 80 kutoka 50 iliyopo sasa.

Dk. Gwajima ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam, wakati akifungua kikao kazi cha kujadili udhibiti wa upotevu wa dawa na vifaa tiba nchini, kilichowajumuisha wadau wanaohusika na mnyororo wa ugavi wa dawa na vifaa tiba, wakiwemo Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bohari ya Dawa (MSD) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

“Suala la upatikanaji wa dawa siyo ajenda ya bajeti pekee, bali ni ajenda ya uwajibikaji wa kizalendo na nidhamu thabiti ya uongozi kwenye usimamizi sehemu ya kazi tukiyatafsiri hayo kazi yetu itakuwa nyepesi,” amesema

error: Content is protected !!