Watoto wafanyiwa majaribio ya chanjo ya UVIKO-19

HomeKimataifa

Watoto wafanyiwa majaribio ya chanjo ya UVIKO-19

Wakati mataifa yote duniani yanaendelea na mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO 19) kwa kuhakikisha watu wanaendelea kupatiwa chanjo duniani kote, bado tafiti zinaendelea kufanyika kuhakikisha kwamba ugonjwa huo hauendeleii kuathiri maisha ya binadamu pamoja na shughuli zake.

Kuna baadhi ya chanjo ambazo zimeanza kutolewa kwa watu wazima zikiwa zinatengenezwa na mataifa mbalimbali na zimeidhinishwa na Shirika la Afya Dunia (WHO) kama Sinopharm, Sinovac-Coronavac, Jassen, Oxford/Astrazeneca, Moderna na Pfizerbiontech.

Lakini watafiti wameamua kugeukia upande wa watoto na kuhakikisha wanakuwa salama kwa kupatiwa chanjo. Mapacha Lizzy na Evan, watoto wa John wenye umri wa miaka saba kutokea Marekani wamepelekwa kwenye kliniki ya majaribio ya chanjo ili kusaidia mchakato wa utengenezwaji wa chanjo kwa ajili ya watoto kati ya miaka 5 hadi 11.

Sambamba na hilo, watoto hao wanapata neema ya kuwa wanapatiwa damu, miaka miwili ya kuangaliwa kwa ukaribu pamoja na kuwa wanapata vipimo vya UVIKO 19. John amesema waliongea na watoto wao ili kuhakikisha wanaelewa na kukubali kwa hiari yao kwa sababu ni miili yao pia wao hawatilii mkazo kwenye vitu ambavyo watapata kama neema ya kukubali watoto wao kuchanjwa ila wanaamini sayansi.

error: Content is protected !!