Fahamu haya kabla ya kununua hisa kwenye kampuni

HomeBiashara

Fahamu haya kabla ya kununua hisa kwenye kampuni

Kutokana na kukua kwa mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji, suala la uuzaji hisa katika makampuni limekuwa likifanywa na makampuni mengi hapa Tanzania lakini unaweza kujiuliza hisa ni nini?

Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni ambayo kampuni inaamua kuiuza kwa wananchi, serikali au makampuni mengine. Kuna faida ambazo mnunuzi anaweza kuzipata kutoka kwa kampuni kama kupata gawio, mnunuzi wa hisa anapata faida za hisa zake ikiwa thamani ya hisa kwenye kampuni imeongezeka ukilinganisha wakati ananunua na wakati kampuni inapoamua kuuza hisa zake. Pili gawio linaweza kutokana na faida ambayo kampuni inapata kutokana na biashara zake za kila siku.

HAKI NA WAJIBU WA MWANAHISA
Kuhudhuria na kupiga kura kwenye mikutano ya kampuni. Ikiwa kampuni inataka kufanya mabadiliko yoyote lazima mwanahisa ahusishwe.

Ana haki ya kupata tarifa zote za kampuni kutoka kwa wakurugenzi wa kampuni pamoja na taarifa za kupanda na kushuka kwa hisa, uuzwaji wa hisa, kujua faida na hasara ya kampuni pamoja na mwenendo mzima wa kampuni.

Ana haki ya kuuziwa hisa mpya kabla ya wawekezaji wengine ambao hawana hisa kwenye kampuni, ikitokea kampuni inataka kuuza tena hisa zake mmiliki ana haki ya kutaka kuuziwa yeye kwanza kabla ya wawekezaji wengine ambao hawana hisa kwenye kampuni.

HASARA NA KUFILISIKA KWA KAMPUNI KWENYE HISA
Pamoja na yote hayo kama mwekezaji au mmiliki ana haki ya kupata faida ya kampuni pia kama itatokea kampuni itapata hasara basi na wewe mwekezaji unapata hasara ya thamani ya hisa yako kushuka ingawa idadi yake inabaki pale pale, kama unamiliki hisa 10 zitabaki kuwa 10. Ikitokea kampuni imefilisika mwekezaji atasubiri mfilisi ambaye atatokea kuinunua kampuni na kuanza kuuza mali za kampuni, kama kuna fedha ambayo itabakia baada ya kulipa madeni ya kampuni wanahisa watapewa, ila ikitokea hakuna fedha iliyobaki basi mmiliki anakuwa hana anachomiliki tena.

UHAMISHWAJI WA HISA
Mwekezaji au mmiliki wa hisa anaweza kuhamisha sehemu ya umiliki wake kutoka kwake kwenda kwa mtu mwingine ikiwa hisa hizo haziko kwenye mnada, na ni rahisi zaidi kwa Soko la Hisa la Dar es Salaam kutokana na kuhifadhi taarifa zake kwenye mfumo wa dhamana na sio makaratasi.

error: Content is protected !!