Zifahamu faida za bamia kwa wanawake

HomeElimu

Zifahamu faida za bamia kwa wanawake

Bamia ni moja ya zao lenye faida mwilini kama tunda mboga kwani linaweza kukutoa katika hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari kwa sababu ya uwezo wake wa kusaidia kuyeyusha au kumeng’enya sukari na kuuweka sawa mfumo wa sukari mwilini.

Faida nyingine za ulaji wa bamia ni kuondosha vimelea vya sumu kwenye ngozi. Pia inasaidia kuimarisha afya ya nywele na kuongeza kinga ya mwili. Bamia ina kiasi kikubwa cha vitamin C, K na folic acid ambayo husaidia mmeng’enyo wa chakula.
> Vanessa Mdee ashambuliwa kisa wigi alilovaa

Pia, ina vitamini A ambayo inasaidia kutengeneza kinga dhidi ya maradhi na sumu zinazoweza kuingia mwilini. Mbali na hayo, husaidia kulainisha choo na kuongeza hamu ya kula. Inasaidia urahisi wa kumeza chakula na huboresha uwezo wa macho kuona. Kwa wenye uzito uliopitiliza, bamia hupunguza lehemu na kusaidia kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Aidha ulaji wa bamia mara kwa mara kwa wanawake husaidia kuponya kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi na  huongeza kinga ya mwili.

error: Content is protected !!