Akanti za Youtube za msanii gwiji wa muziki wa miondoko ya RnB, R. Kelly zimefungwa mapema wiki hii, ikiwa ni tukio la kwanza kubwa kumfika tangu alipotiwa hatiani kwa makosa mbalimbali nchini Marekani.
Akaunti za msanii huyo zimetolewa hewani kutokana na msanii huyo kukutwa na hatia ya makosa ya unyanyasaji ya kingono kama kunajisi watoto, unyanyasaji wa kijinsia pamoja na makosa ya utakatishaji fedha na rushwa.
Nyimbo za R. Kelly kwa njia sauti (audio) bado zipo kwenye mtandao huo, lakini akaunti zake za ‘RKellyVevo’ na ‘RkellyTV’ zimetolewa hewani tangu siku ya Jumanne wiki hii.
> Mwanamuziki R. Kelly akutwa na hatia
Mwanasheria Mkuu wa mtandao wa Youtube, Nicole Alston amesema kuwa Youtube imechukua uamuzi huo kutokana vitendo vya R.Kelly ambavyo vina madhara makubwa kwenye jamii, na kwamba uamuzi huo ni kulinda watuamiaji wa mtandao wao dhidi ya vitendo hivyo vibaya.
Hata hivyo, wakauti za watumiaji wengine wa YouTube zenye nyimbo za R Kelly zitaendelea kuwa hewani na nyimbo hizo zitakuwepo.