Unapoanzisha mahusiano na mtu, jambo la kwanza hakikisha unajua hayo mahusiano ni ya nini na hatima yake ni nini? Kwa lugha rahisi ni kwamba unapoanzisha mahusiano hakikisha unafahamu ni nini has unakihitaji toka katika mahusiano hayo.
- Mahusiano ya kujionesha (Show off relationship).
Mahusiano haya hayaendi popote bali ni kwa ajili ya ya kujionyesha tu kwa watu kuwa na wewe una mtu wa kukuweka ‘busy’ kimahusiano. - Mahusiano ya kutojiamini (Partial relationship).
Mahusiano haya ni ya kupotezeana muda tu, mwanzilishi wa mahusiano, au aliye katika mahusiano haya hana uhakika kama aliye naye ndiye chaguo sahihi. Kuna wakati anaonesha kuwa chaguo sahihi lakini kuna wakati anakuwa na wasiwasi hadi kutaka anataka kusitisha mahusiano ila anakosa namna ya kusitisha.
> Dakika tano zinatosha kumfikisha mwanamke kileleni
- Mahusiano ya ngono (Sexual relationship).
Mahusiano haya yanadumu kwa kutimiziana mahitaji ya kimwili. Hapa mara nyingi hutumika maneno na ahadi ya kuoana kwa kuwa nimejua uzuri wako, ladha yako na sitakuacha, lakini ukweli wake, pale Mwanamke anapoonesha hitaji la “commitment” kama kujitambulisha kwa wazazi n.k kijana humzungusha, kuanza vituko na hata kukata mawasiliano. - Mahusiano ya kitoto (Childish relationship).
Mahusiano haya wahusika ni kama watoto, wanatumia gharama, zawadi, muda, kuitana majina ya kama mtarajiwa, kuambizana nakupenda lakini wanaweza maliza hata miaka 5 bila chochote. Katika mahusiano haya hakuna hatua, mipango maalumu inayoonesha dalili za wahusika kuingia kwenye ndoa. - Mahusiano ya ndoa (Marriage relationship).
Haya ni mahusiano muhimu, yenye mipango, malengo, heshima, kulinda hisia, kulinda heshima na yenye kumtanguliza Mungu. Hapa mhusika mkuu ambaye kimsingi ni Mwanaume hutoa mwelekeo wa kuekekea kwenye ndoa, huonesha harakati za michakato mahsusi ya kuingia katika ndoa. Wakati huo huoMwanamke humtia moyo mwenza wake na kumuonesha ushirikiano wa namna inavyowezekana kufikia mipango yao.
NB: Wewe upo kwenye aina gani ya mahusiano?