Rugemalira arudi Mahakamani tena

HomeKitaifa

Rugemalira arudi Mahakamani tena

Mfanyabiashara James Rugemalira, ameanza harakati za kufungua mashtaka dhidi ya taasisi anazozituhumu kuhusika katika wizi wa trilioni 61 za Serikali zilizomsababishia kesi ya uhujumu uchumi.

Rugemalira ambaye alikaa mahabusu kwa miaka nane na miezi mitatu, amewasilisha maombi ya kibali cha kufungua na kuendesha mashtaka dhidi ya taasisi hizo ambapo maombi hayo yanatarjiwa kusikilizwa Novemba 10 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kampuni na taasisi zinazotuhumiwa na Rugemalira ni  Benki ya Standard Chartered (Hong Kong), Benki ya Standard Chartered Tanzania, Benki ya Standard Chartered Berhad (Malysia), Wartsila Tanzania Limited na Wartsila Netherlands BV.

Rugemalira pia anakusudia kuwashtaki Abrar Anwai (Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered nchi Malysia),  Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Chartered (Hong Kong) Samir Subbrwai, Sanjay Rughani (Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Tanzania0, Bill Winters (Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered) ma Hakan Agvell ambaye ni Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wartsila Corporation.

Rugemalira anaituhumu kampuni ya Mechmar ambayo ilikuwa mbia mkuu wa IPTL kula njama na benki ya Standard Chartered kukwepa kulipa dola milioni 4.2 za Kimarekani ambazo ni asilimia nne ya ushuru wa forodha katika mkopo wa IPTL wa dola milioni 105 za Juni 28,1997.

Rugemalira anasema anakusuduia kufungua mashtaka hayo kwa lengo la kurejesha shilingi trilioni 61 ambazo benki ya Standard Chartered na washirika wake walifanya ulaghai kuzichepusha kutoka kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na VIP Engineering (kampuni ya Rugemalira) isivyo halali.

error: Content is protected !!