Mwanafunzi wa shule ya msingi ajinyonga

HomeKitaifa

Mwanafunzi wa shule ya msingi ajinyonga

Mwanafunzi wa shule ya Msingi Lukobe, Egdius Edmund mwenye umri wa miaka 13 mkazi wa mtaa wa Tushikamane Manispaa ya Morogoro amekutwa amejinyonga hadi kufa chumbani kwa dada yake, kwa kutumia kamba ya manila.

Dada wa Marehemu anaejulikana kama Editha Edmund, alikua mtu wa kwanza kushuhudia tukio hilo. Editha anasema alimwambia mdogo wake waende Kanisani ila mdogo wake huyo alikataa na kusema anabaki nyumbani kwa ajili ya kufanya kazi zake za shule yaani homework ndipo Editha aliondoka na kumuacha mdogo wake nyumbani.

Nyumbani hakukua na mtu mwingine wakati baba wa watoto hao alikua kazini. Baada ya tukio baba wa mtoto huyo Edmund Peter alisema mwanaye hakuwa na tatizo lolote la kiakili, alikua mtu wa furaha muda wote na kwamba tukio hilo linawapa maswali mengi kujua nini kilimsibu kijana huyo.

Mwenyekiti wa mtaa huo Omary Hassan alisema kuna haja ya wazazi kuwa karibu na watoto wao, Alisema huenda sababu ni watoto kuishi na baba yao huku mama akiishi sehemu nyingine na mtoto huyo kushindwa sehemu ya kufikisha tatizo lililokua linamkabili.

error: Content is protected !!