Polisi nchini Uganda wameua watu watano na kukamata wengine 21 wanaoshukiwa kuhusika kwenye milipuko miwili ya mabomu iliyotokea juma lililopita ambapo watu zaidi ya watano walifariki, watu hao wanahusishwa kuwa wanamgambo wa kundi la ISIS.
Askari kikosi cha kupambana na ugaidi nchini Uganda waliua watu hao eneo la Ntoroko walipokuwa wanajaribu kuvuka mpaka kukimbilia DRC. Mmoja aliweuwawa ni Sheikh Abas Muhamed Kirevu, aliuwawa wakati akijaribu kutoroka, na Kirevu ni kiongozi wa dini anayesemekana kuhusika na shambulio la jijini Kampala,
Jeshi la Polisi nchini Uganda limesema kuwa watu 21 waliotiwa mbaroni ni watu wa kundi la ADF, kundi la waasi lenye maskani yake mashariki mwa DRC ambalo idara ya usalama Marekani inasema kuwa kundi hilo lina uswahiba na kundi la ISIL.
Baada tu ya shambulio hilo ADF walisema wanahusika na tukio hilo katika eneo la Kawempe Kampala