Wasichana waliopata ujauzito kuruhusiwa kurudi shuleni

HomeKitaifa

Wasichana waliopata ujauzito kuruhusiwa kurudi shuleni

Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako amesema kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, Serikali imeamua kuondoa vikwazo vilivyopo katika elimu hususani kwa watoto wa kike katika elimu ya sekonadari na elimu ya msingi.

Profesa Ndalichako amesema Serikali imeadhimia kwamba wanafunzi wa kike wanaopata mimba warudi shuleni baada ya kujifungua ambapohii ni kwa wanafunzi wote wa Sekondari na Shule za msingi.

Pia wanafunzi ambao wanapata changamoto wakati wa mitihani ya darasa la saba ikiwemo udanganyifu na kufeli watapatiwa nafasi ya kurudia mitihani yao na endapo watafaulu wataeza kupangiwa shule za serikali.

Kabla ya kutolewa kwa kauli hiyo leo na Prof Ndalichako wanafunzi wanaofeli darasa la saba walikua hawana nafasi ya kurudia mtihani, lakini pia wanafunzi wa kike waliokua wanapata mimba shuleni walikua hawartuhusiwi kurudi shule hata baada ya kujifungua.

error: Content is protected !!