GSM amkalia kooni Makonda

HomeKitaifa

GSM amkalia kooni Makonda

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anadaiwa kutaka kupora nyumba ya mfanyabiashara Gharib Said Mohamed wa kampuni ya GSM.

Nyumba hiyo iko kati ya maeneo ya Oysterbay na masaki Jijini Dar es Salaam, Makonda anadaiwa kusuka mipango ya kuchukua nyumba hiyo akiwa madarakani.

Nyumba hiyo imeingia kwenye mgogoro mzito baada ya Makonda kuendelea kudai kuwa nyumba hiyo ni ya kwake, huku Gharib nae akidai ni ya kwake.

Watu wa karibu na Gharib wanasema Nyumba hiyo iliporwa na baadae ilirejeshwa mikononi mwa Gharib miezi mitano baada ya utawala wa nchi kubadilika.

Kwa upande wa Makonda ameonekana kwenye moja ya video inayosambaa mtandaoni akilalamika mbele ya askari wa jeshi la Polisi, Makonda alikua akilalamika kuwa ni mali yake na amenunua kiwanja mwaka 2018 na kuanza kujenga na kila kinachoonekana katika jengo hilo ni mali yake na risiti anazo.

“Fanyeni mnaloweza, lakini mimi ndio mwenye mali na hivyo siwezi kukubali. Nimekaa kwenye mkoa huu sijawahi kudhurumu watu. Sitakubali viongozi wote wanafahamu kuwa hii ni mali yangu” alisema Makonda.

Mkuu wa mkoa huyo wa zamani anasema uhamishwaji wa umiliki huo umeanza Januari  mwaka huu, wakati yeye akiendela na taratibu za kawaida za kulifuatilia eneo hilo na kuomba mamlaka kuingilia kati kuangalia nani anayehusika na umiliki huo.

Katika sakata hilo Makonda nadai kuvamiwa na kutishiwa risasi ndipo alipotafutwa Kamanda wa Polisi kanda ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema mashtaka yanayohitaji kuchunguzwa na jeshi la polisi hayafunguliwi kwenye mitandao vituo vya polisi vipo akafungue mashtaka.

Wakati akiwa Mkuu wa Mkoa, Makonda alikua na ukaribu mkubwa sana na mfanyabiashara Gharib, cheo cha ukuu wa mkoa kwa Makonda kilikoma mwaka 2015 baada ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kugombea ubunge katika jimbo la Kigamboni ambapo alikosa nafasi hiyo ambayo ilichukuliwa na Dk Faustine Ndungulile.

Kwa sasa Makonda anakabiriwa na mashtaka yaliyofunguliwa na Mwandishi wa habari Saed Kubenea, Katika mashtaka hayo makonda anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka akiwa mkuu wa mkoa ikiwemo kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds.

error: Content is protected !!