App mbili unazoweza kuzitumia badala ya WhatsApp

HomeBiashara

App mbili unazoweza kuzitumia badala ya WhatsApp

Tovuti nyingi ulimwenguni ikiwemo Bloomberg na Independent zimeandika kuhusu mitandao inayokimbiliwa kama mbadala wa WhatsApp kila mtandao huo unapopata matatizo.

Hapo jana mitandao ya Facebook, WhatsApp, na Instagram ilitoweka hewani kwa takribani kwa saa 6 na kuwakosesha huduma wateja wake wasiopungua bilioni 2.7 ulimwenguni kote. Matatizo yaliyoipata kampuni ya ‘Facebook Inc’ yalikuwa faida kwa wapinzani wao hususani Twitter.

Mamilioni ya watu walipakua ‘application’ ya Signal huku Telegram ambayo matumizi yake yanafanana kwa kiasi kikubwa na Whatsapp ikipata kwa zaidi ya nafsi 55 kwenye orodha ya ‘application’ zilizopakuliwa na watumiaji wa iPhone nchini Marekani (kwa mujibu wa tovuti ya Sensor Tower)

 > Fahamu kwanini Facebook, Instagram na Whatsapp zilitoweka hewani

Kupitia Twitter, Mtendaji Mkuu wa Twitter, Jack Dorsey  ameandika sentensi moja iliyolenga kuwaonesha watu kwamba Signal ndio mbadala wa WhatsApp. Ameandika “Signal is WhatUp”, jambo ambalo limetajwa kupepeleka watu wengi kwenye mtandao wa ‘Signal’ unaodaiwa kujikita zaidi kwenye usiri wa watumiaji wake.

Kwa upande wa Telegram kupata watumiaji wengi kila WhatsApp inapopata matatizo imekuwa kawaida. Mfano,  Machi 13, 2019, baada ya WhatApp kuwa na matatizo ya kimtandao, muazilishi wa Telegram, Pavel Durov alisema “Naona watumiaji wapya milioni 3 wamejiunga na ‘Telegram’ ndani ya saa 24 zilizopita.”

Signal na Telegram zimeonekana kuwa mbadala wa WhatsApp, kila WhatsApp inapopata matatizo ya kimtandao ama kutokana na madai ya kwamba Signal na Telegram zimezingatia zaidi usiri wa mtumiaji.

 

 

error: Content is protected !!