Askari adawa kumuua mwenzake kisa mwanamke wakiwa lindoni

HomeKitaifa

Askari adawa kumuua mwenzake kisa mwanamke wakiwa lindoni

Askari Polisi Onesmo Joseph, amefariki baada ya kupigwa risasi na askari mwenzake wakiwa lindo katika Benki ya CRDB, tawi la Ruangwa mkoani Lindi. Tukio hilo lilitokea December 9 majira ya saa 6 mchana katika tawi hilo lilioko mtaa wa Mchangani mjini Ruangwa mkoani humo.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi , Mtatiro Kitinkwi alidai askari mwenye namba H.2324 alietajwa kwa jina moja la Joseph alimpiga risasi askari mwenzake na kumjeruhi sehemu za nyonga katika mguu wa kulia baada ya kutokea mtafaruku baina yao.

Kamanda Mtatiro alisema chanzo cha ugomvi wao bado hakijafahamika huku baadhi ya watu wakidai walikua wanagombea mwanamke wengine wakidai chanzo ni pikipiki, pia aliongezea kuwa Onesmo alifariki dunia akiwa njiani kukimbizwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam kwaajili ya kuendelea na matibabu.

Aidha alisema tayari askari huyo ameshafukuzwa kazi na anandaliwa utaratibu wa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji ya askari mwenzake, pamoja na hayo aliwataka askari wake kuacha tofauti zao na badala yake waendelee kujenga umoja na upendo kwa usalama wao na jamii pia.

error: Content is protected !!