Baba yake Lupita ashinda uchaguzi Kenya

HomeKimataifa

Baba yake Lupita ashinda uchaguzi Kenya

Mwigizaji aliyeshida tuzo ya Oscar, Lupita Nyong’o jana Agosti 11,2022 amempongeza baba yake kwa kushinda muhula wa pili na wa mwisho kama gavana wa kaunti ya Kisumu nchini Kenya.

Baba yake, Anyang Nyong’o, alitangazwa mshindi Jumatano baada ya kura za uchaguzi mkuu wa kenya siku ya Jumanne.

Muigizaji huyo aliyeshinda tuzo ya Oscar alilelewa nchini Kenya, kabla ya kuhamia Marekani.

Nyong’o ambaye alishinda mwigizaji bora msaidizi kwenye tuzo za Oscar kutokana na filamu iitwayo 12 Years a slave, aliwashukuru watu wa Kisumu kwa ‘msaada wao mkubwa ‘ kwa baba yake kwenye uchaguzi.

error: Content is protected !!