Catherine Ruge wa Chadema akamatwa

HomeKitaifa

Catherine Ruge wa Chadema akamatwa

Catherine Ruge ambaye ni Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa, amekamatwa na polisi Mkoa wa Mara muda mfupi kabla ya kuongea na waandishi wa habari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Longinus Tibishibwamu ameeeleza kuwa wamemkamata Ruge ili kumhoji kutokana na kuandika tuhuma mbalimbali dhidi ya Jeshi la Polisi alizokuwa akitoa katika mitandao ya kijamii baada ya kuuawa kwa watu watatu juzi Wilaya ya Serengeti wanaodaiwa kuwa ni majambazi, akiwemo mjomba wa Ruge.

error: Content is protected !!