Muimbaji nguli wa muziki wa sauti za pole pole katika aina za muziki za pop, chanson pamoja na Soft Rock, Celine Dion, anakabiliwa na ugonjwa usiweza kutibika na unaoshindwa kuuruhusu mwili wake kutembea na kuimba katika sauti yake halisi aliyebarikiwa mwanamuziki huyo aliyezaliwa tarehe 30 Machi 1968 huko Charlemagne, Quebec nchini Canada.
Hivi karibuni, Celine aliweka wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram kua anakabiliwa na maradhi ya ‘Neva’ yasiyoweza kupatiwa matibabu yanayojulikana kama Stiff Person Syndrome (SPS), na kusema kua maradhi hayo ni ya muda mrefu kwake isipokua sasa yameanza kumzuia kufanya shughuli zake za kawaida za kila siku.
“Nimegundulika kua na ugonjwa wa Neva unaojulikana kama Stiff Person Syndrome (SPS) ambao kwa wastani hua unaathiri mtu mmoja kati ya watu milioni moja duniani. Kwa bahati mbaya ugonjwa huu unaniathiri katika maisha yangu ya kila siku. Kuna wakati ninapata ugumu wa kutembea pia hauniruhusu kutumia sauti yangu ya kawaida niliyoizoea katika uimbaji wangu” Alisema Celine.
Mwimbaji huyo wa vibao maarufu vya ‘New days has come’, My heart will go on’ Love don’t ask why na vingine vingi ni miongoni mwa wanamuziki nguli duniani waliofanikiwa kufanya kazi za muziki na kutambulika duniani kote akitajwa katika ushindaniwaji wa tuzo mbalimbali duniani zisizopungua mia nne na themanini na moja (481) na kushinda tuzo zisizopungua mia mbili na arobaini (240).