Chanzo cha ajali ya basi Sikonge

HomeKitaifa

Chanzo cha ajali ya basi Sikonge

Majeruhi 13 kati ya 48 wa ajali ya basi la Sasebosa iliyotokea wilayani Sikonge wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kupatiwa matibabu na afya zao kuimarika.

Ajali hiyo ilitokea jana Ijumaa Julai Mosi, 2022 jioni katika kijiji cha Mabangwe wilayani Sikonge mkoani Tabora na kusababisha vifo vya watu watano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema basi hilo lilikuwa linatoka mkoani Mbeya kwenda Tabora.

Kwa mujibu wa mganga mfawidhi Hospitali teule ya Sikonge, Dk Peter Songoro amesema majeruhi 29 bado wapo katika Hospitali ya Wilaya ya Sikonge, watano wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete huku mmoja akipelekwa katika Hospitali ya Malolo.

Katika Vifo vilivyotokea mwanaume ni 1 wanawake 3 na mtoto mmoja wa kike.

Chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa kuwa ni kupasuka kwa tairi la mbele la basi hilo.

error: Content is protected !!