Yanga haina mpinzani

HomeMichezo

Yanga haina mpinzani

Baada ya vuta n’kuvute  kwa dakika 120 kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Sheikh Abeid jijini Arusha hatimaye bingwa wa kombe la shirikisho la Azam amepatikana.

Mechi hiyo ilifika hatua ya matuta baada ya sare ya goli 3-3 huku Yanga akitokea nyuma mara mbili kufikia hatua ya penalti.

Ushindi wa 4-1 kwa changamoto za penalti zilitosha kuisaidia Yanga kutangaza ubingwa wa FA mbele ya Coastal Union.

Yanga SC msimu wa 2021/22 imeshinda 

-Ngao ya Jamii

-Ligi Kuu Tanzania Bara

-Kombe la Shirikisho Tanzania

 

 

error: Content is protected !!