DC Jokate ashtukia madudu Temeke

HomeKitaifa

DC Jokate ashtukia madudu Temeke

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Temeke, Herieth Makombe amesimamishwa kazi kwa muda na Mkuu wa Wilaya hiyo, Jokate Mwegelo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mikopo ya makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

“Nimeshangaa sana madudu yaliyofanyika katika mikopo hii, ni kwa nini hadi sasa ofisa maendeleo ya jamii bado upo katika nafasi yako,”

“Wengi wanapenda nafasi ziwatumikie kuliko kuzitumikia nafasi zao, nasema hayo sababu lazima tujitafakari katika uongozi wetu,” alisema Jokate.

Mhe. Jokate alichukua uamuzi huo wakati akipokea ripoti maalumu ya ukaguzi wa fedha za mikopo ya halmashauri ya Temeke, ambapo alisema baada ya uchunguzi watakaokutwa na hatia hatua za kisheria zitachukulia dhidi yao.

 

error: Content is protected !!