Waziri Nape aeleza maagizo ya Rais Samia kwa Wanahabari

HomeKitaifa

Waziri Nape aeleza maagizo ya Rais Samia kwa Wanahabari

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewaeleza wahariri wa vyombo vya habari muelekeo wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye tasnia ya habari ikiwemo kujenga mahusiano mazuri baina ya serikali na wanahabari.

“Serikali ya awamu ya sita tunataka tuboreshe mahusiano yaliyopo, na mimi najua tulikotoka tuboreshe mahusiano yaliyopo na kila wakati tuendelee kuboresha mahusiano kati ya wanahabari, sekta ya habari na Serikali tuyaboreshe kadri inavyowezekana,” Mhe. Nape Nnauye.

Licha yakuboresha mahusiano kati ya Serikali na wanahabari, Waziri Nape alisema kwamba Rais Samia amewataka kupitia upya sheria, kanuni, sera na taratibu zinazosimamia sekta ya habari.

“Mhe. Rais ameelekeza tupitie sheria, sera, kanuni na taratibu zinazosimamia sekta hii ya habari na tuone namna yakuzifanya ziwe rafiki na kuwezesha utendaji kazi wa wanahabari badala ya kuwa sehemu ya kikwazo ya shughuli za wanahabari,” Mhe. Nape Nnauye.

Aidha, Waziri Nape amevifungulia na kutoa leseni kwa magazeti 4 yaliyokuwa yamefungiwa ambayo ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima huku akiongezea kwa kusema kuwa ni njia moja wapo yakufungua ukurasa mpya. 

 

error: Content is protected !!