Baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kutoa taarifa kuhusu ugonjwa wa Homa ya Mgunda (Leptospirosis), wizara hiyo imetoa tahadhari kwa wananchi na njia za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.
Njia za maambukizi ya ugonjwa wa homa ya mgunda
1. Kugusa mkojo au majimaji mengine ya mwili kutoka kwa wanyama wenye maambukizi (Panya, Kindi, Mbweha, Kulungu, Swala na Wanyamapori wengine)
2. Kugusa maji, udongo au chakula kilichochafuliwa na mkojo wa wanyama wenye maambukizi.
3. Kunywa maji yaliyochafuliwa na vimelea vya bakteria wa ugonjwa huu.
Vilevile ugonjwa wa Homa ya Mgunda (Leptospirosis) huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia uchafuzi wa maizngira ikiwemo vyanzo vya maji kutoka katika mkojo wa wanyama wenye maambukizi.
Dalili za Ugonjwa wa Homa ya Mgunda (Leptospirosis)
1. Homa kali
2. Kuumwa kichwa
3. Maumivu ya misuli
4. Uchovu wa mwili
5. Kupata rangi ya manjano hasa kwenye macho
6. Macho kuvilia damu
7. Kukohoa/kutokwa na damu puani
8. Kichefuchefu, kutapika, kuharisha na tumbo kuuma