Hamisa Mobetto na Rick Ross mambo sio siri tena

HomeBurudani

Hamisa Mobetto na Rick Ross mambo sio siri tena

Mwanamitindo na msanii kutoka nchini Tanzania, Hamisa Mobetto ameonekana akiwa na wakati mzuri huko Dubai pamoja Rapa kutoka nchini Marekani Rick Ross, ambapo wawili hawa kulikua na uvumi kuwa wako kwenye mahusiano baada ya kuonekana kuonyesha ukaribu miezi michache iliyopita.

Mwezi Septemba mwaka huu Rick Ross aliulizwa kuhusu mahusiano yake na mrembo huyo na kusema kwamba anamuachia Hamisa kuweka wazi kwa kinachoendelea kati yao huku akimtaja kama mwanadada anayejituma na kutaka kumsaidia kufika mbali.

“Kusema ukweli kuna kitu kinaendelea kati yetu ila nitamuachia yeye aweke wazi na kuongelea suala hili, Hamisi ni mrembo na mchapakazi hivyo basi nataka kumsaidia pia kumfikisha mbali,” alisema Rick Ross.

Jana wawili hao wameonekana wakiwa pamoja baada ya Hamisa kuweka kwenye ukurasa wake wa Instagram video wakiwa wanacheza na kujivinjari jambo linalokamilisha uvumi kwamba wapo kwenye mahusiano ya muda mrefu na sasa wameamua kuweka wazi juu ya mahusiano hayo.

error: Content is protected !!