Aliyekuwa Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) ni kati ya Wabunge waliochangia hoja hiyo wakimuomba Spika wa Bunge atoe mwongozo kuhusu utajiri huo wa Makonda ndani ya muda mfupi.
Kwa mujibu wa wabunge hao, Makonda alinunua ‘apartment’ katika majeno ya ‘Viva Towers’ jijini Dar es Salaam kwa shilingi milioni 600, alimpa mke wake gari aina ya Mercedes Benz lenye thamani ya Dola 250,000 za Marekani (Takribani shilingi milioni 550) kama zawadi ya ‘Birthday’, alikuwa na anamiliki gari aina ya Lexus, lenye thamani ya shilingi milioni 400.
>Paul Makonda kufikishwa Mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka
Mbali na mali hizo Msukuma alisema Makonda anamiliki magari mengine ya kifahari aina ya V8, amejenga maghorofa jijini Mwanza na alikarabati ofisi yake kwa shilingi milioni 400 bila kutumia utaratibu wa sheria ya manunuzi.
Leo (Novemba 15,2021) gazeti la Raia Mwema limeandika kwamba, Makonda anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.Habari hiyi imezua mijadala sehemu mbalimbali, ikiwa ni siku chache baada Lengai Ole Sabaya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, kuhukumiwa kufungo cha miaka 30 jela kufuatia kukutwa na hatia katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka.