Kitambi ni moja ya tatizo linalowakwaza wengi na kuharibu muonekano wa mtu pale anapovaa nguo za aina fulani na wengi hutafuta namna ya kuondoa kitambi lakini kukata tamaa njiani.
Hizi ni njia rahisi ambazo zitakupatia majibu ya kitambi chako haraka zaidi
Kunywa maji ya mdalasini kila siku asubuhi kabla ya kula kitu chochote,. Chemsha mdalasini kijiko kimoja cha chai kwenye maji kikombe kimoja na nusu vikichemka mimina kwenye kikombe, changanya asali kijiko kimoja na limao kijiko kimoja cha chakula kisha kunywa.
Sit-ups na planks
Haya ni mazoezi ambayo hukata mafuta kwenye tumbo na kuliweka kwenye shape nzuri kwa wale wanaotafua Abs. Fanya seti mbili ya Sit-ups 10 na kisha planks 10 walau mara mbili kwa siku na uende ukiongeza idadi mara kwa mara.
Hakikisha unakula kabla ya saa mbili usiku. Hii ni kuupa mwili nafasi ya kumeng’enya chakula huku bado ukiwa na nguvu. Unapokula saa tatu siku mwili na akili huwa vimechoka na unapolala mwili kushindwa kumeng’enya chakula inavyopaswa na kupelekea mtu kupata kitambi. Vilevile jitahidi kula vyakula vyepesi wakati wa usiku
Punguza kula vyakula vya wanga kama vile ugali, chapati, wali makande na kula vyakula vya protini zaidi kama vile samaki, mayai, maziwa, nyama, soya. Pia kula matunda na mboga mboga.
Acha kutumia sukari. Sukari pekee utayotumia iwe ni ya matunda. Matumizi ya soda, sharubati za madukani, yote acha kwani sukari hiyo hubadilika kuwa mafuta mwilini na kuchangia kwenye kuongezeka kwa kitambi.