Jinsi ya kurudisha ‘meseji za WhatsApp’ ulizofuta

HomeElimu

Jinsi ya kurudisha ‘meseji za WhatsApp’ ulizofuta

‘WhatsApp’ ni mtandao unaotumiwa na wengi zaidi katika mawasiliano ya kila siku.

Kwa bahati mbaya, unaweza kujikuta umefuta ‘meseji’ (ujumbe0 ambayo hukutaka kuifuta kwenye WhatsApp yako, au umeifuta lakini baada ukatamani kuirejesha.

Usijali, kuna uwezekano wa kurudisha ‘meseji’ uliyofuta kwa bahati mbaya.

Jambo la kwanza unalotakiwa kufanya ili kuhakikisha kwamba ‘meseji’ utakazofuta kwenye simu yako zinaweza kurejea, ni kufanya ‘Chat Backup’.

Nenda sehemu ya ‘Settings’ utaweza kuona sehemu ya ‘Backup’ ambapo unaweza kuchagua kufanya ‘Backup’ kwa siku (Daily), kwa wiki (Weekly) kwa mwezi (Monthly) au usifanye (Off).

‘Backup’ zinazofanywa kwa siku (Daily) zitakusaidia kurejesha kwa urahisi ujumbe uliofuta siku hiyo, wakati ‘Backup’ za wiki zitafanya simu yako irejeshe ‘meseji’ ambazo zilikuwa kwenye simu yako kwa kipindi cha takriban siku sita zilizopita na kutengeneza uwezekano wa kukosa ujumbe ulioufuta muda mfupi uliopita.

Jinsi ya kurudisha ‘meseji’

Futa (unistall) ‘WhatApp’ yako kisha uiweke upya (Install).

Utapokea ujumbe wa kukuuliza kama kurejesha (Restore) historia ya meseji zako.

Ruhusu (Restore) na ‘meseji’ zilizokuwepo ulipofanya ‘backup’ ya mwisho zitarudi.

Hii inafanya kazi kwa simmu za ‘Android’ na ‘iOS’ lakini inategemeana nauchaguzi wako wa muda wa kufanya ‘backup’.

 

error: Content is protected !!