Katiba sio tatizo, Watanzania hatujui tunataka nini

HomeKitaifa

Katiba sio tatizo, Watanzania hatujui tunataka nini

Kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa tangu kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ugaidi, kumekuwapo na sauti nyingi kutoka kwa wanaharakati, wanazuoni na wafuasi/wanachama wa chama hicho wakidai kuwa Mbowe si gaidi. Hilo hakuna anayelikataa, kwani inafahamika kuwa Mbowe ni mtuhumiwa wa ugaidi, sio gaidi, hadi hapo mahakama itakapoamua vinginevyo.

Lakini sauti hizi hazikuishia hapo, zimekwenda mbali na kumtaka (sio kumuomba) Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati kesi hiyo ili Mbowe aweze kuachiliwa. Hili linawazisha na kutafakirisha sana, hasa juu ya ni kitu gani sisi Watanzania tunakitaka, na uelewa wetu kuhusu utawala wa sheria.

Watu au baadhi yao ambao leo wanamtaka Rais kukiuka katiba na kuingilia muhimili wa mahakama ili Mbowe aachiwe ndio hao hao walipaza sauti kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa wakidai kuwa serikali ya awamu ya tano ilikuwa ikiingilia muhimili wa mahakama na kushawishi hukumu au maamuzi ambayo yalikuwa yakitolewa.

Akizungumza na BBC, Rais Samia alionesha wazi kuwa hataki kuvunja katiba kwa kusema kuwa suala hilo lipo mahakamani, hawezi kulizungumzia sana na kwamba mahakama iachwe ifanye kazi yake. Lakini wanaharakati wakamuita kila walichoona kinafaa kwa sababu tu katiba imeheshimiwa na kwa kuheshimiwa huko anayeathirika ni mpendwa wao.

Nimalize kusema kuwa, sakata hili la Mbowe na wanaharakati limenifanya niamini kwamba, katiba si tatizo, bali sisi Watanzania ndio tatizo, kwa sababu tuko tayari katiba ivunjwe endapo matakwa yetu yatafanikiwa, lakini ikiwa si matakwa yetu, basi hatutaki. Kama hatuwezi walau kuheshimu katiba hii ‘mbovu’ tuliyo nayo, hata tukipata ‘mpya’ hatuwezi kuheshimu, kwa sababu TATIZO SIO KATIBA

COMMENTS

error: Content is protected !!