Madhara ya kuvaa mawigi

HomeKitaifa

Madhara ya kuvaa mawigi

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ngozi kutoka Hospitali ya Lugalo, Dk. Msafiri Kombo, alisema kitendo cha wanawake kuvaa mawigi ambayo tayari yameshavaliwa kina madhara liafya kwa kuwa kiansababisha magonjwa ya ngozi na kuambukizana ikiwamo fangasi na mba na wadudu kama chawa.

“Hatari ya kuvaa wigi lililovaliwa na mtu mwingine ipo sehemu mbili, hapo mtu anaweza kupata maambukizi ya fangasi au wadudu wanaopenda kukaa kwenye nywele ikiwamo chawa kama litakuwa halijasafishwa na vifaa vinavyoangamiza vimelea vyake,” alitahadharisha Dkt. Kombo.

Ameshauri wanawake wanaopenda urembo huo kuacha kuvaa vitu vilivyovaliwa na watu wengine ikiwamo nguo na mawigi ili kujiepusha na magonjwa ya ngozi yanayoambukizwa.

“Kikubwa wajitahidi wanunue yao wenyewe, kuazimia nguo, viatu na mawigi haishauriwi kiafya, ni muhimu kila mmoja hasa wananwake kuwa makini na vitu kama hivyo kwa sababu wanapoambukizwa wao ni rahisi kuambukiza watu walio ndani ya familia ikiwamo watoto ambao wanakuwa nao kwa ukaribu,” alisema.

 

error: Content is protected !!