Serikali kunongesha sekta ya maziwa

HomeKitaifa

Serikali kunongesha sekta ya maziwa

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulgea amesema seriklai imejipanga kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya maziwa ili iweze kutoa fursa nyingi za ajira kwa vijana na wanawake.

“Msimamo wa serikali ni kuona uwekezaji katika sekta ya maziwa unashamiri ili zao hilo kiweze kuongezewa thamani na kwa kufanya hivyo wananchi wengi wataweza kujipatia kipato kupitia mnyororo wa thamani,

“Tumepeleka mapendekezo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuondoa kodi nyingi ambazo zikiondoka zitanawirisha tasnia ya maziwa,kwa mfano, kodi zinazohusu vifungashio ili wawekezaji waweze kuzalisha kwa gharama nafuu na kukuza ajira kwa jamii,” alisema Ulega.

Alisema serikali imedhamiria kukutana na wadau wa tasnia ya maziwa kujadili nini kifanyike ili maziwa mengi yanayozalishwa na wafugaji yaende viwandani kwa ajili ya kuchakatwa na kuongezewa thamani.

Aidha, Naibu Waziri huyo alisema serikali itaweka vituo vya kukusanya maziwa sehemu mbalimbali nchini na mwaka huu imetenga bajeti ya kutosja kwa ajili ya kazi hiyo kwa kushirikiana na wadau ili maziwa mengi yaweze kukusanywa na kuingia viwandani.

 

error: Content is protected !!