Madini yachangia 11.9% kwenye Pato la Taifa

HomeKitaifa

Madini yachangia 11.9% kwenye Pato la Taifa

Serikali imesema mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa umeongezeka kutoka 10.1% kwa mwaka 2024 hadi 11.9% kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka 2025 (Januari –Septemba).

Akiwasilisha Mapendekezo ya Bajeti ya Wizara ya Madini bungeni jijini Dodoma leo Aprili 27, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema hatua hiyo imechangiwa na kuimarika kwa usimamizi wa sekta hiyo na kuongezeka kwa uwekezaji na uzalishaji.

Mavunde amesema jitihada za kufanya tafiti, kutangaza fursa za uwekezaji, na kutoa leseni za utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, uyeyushaji, usafishaji na biashara ya madini muhimu na madini mkakati zilizopo zinaendela ili kuhakikisha madini yananufaisha taifa.

“Aidha, wizara inaendelea na taratibu za kuidhinishwa orodha ya madini muhimu na madini mkakati Tanzania ili iweze kutumika katika usimamizi wa rasilimali za madini hayo,” amesema Mavunde.

error: Content is protected !!