Makonda kizimbani Desemba 3

HomeKitaifa

Makonda kizimbani Desemba 3

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Christian Makonda anatarajia kufikishwa Kortini tarehe 3 Desemba mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kinondoni jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka ya jinai yanayomkabili.

Makonda anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali aliyoyatenda wakati wa utawala wa awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, ikiwamo kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds Machi mwaka 2017 na kuingilia mahudhui ya matangazo ya kituo hicho cha habari, matumizi mabaya ya madaraka na ukandamizaji wa haki za binadamu.

Mahakama imetoa wito wa kumtaka afike mahakamani siku hiyo ya tarehe 3 Desemba mwaka huku ikiwa ni mara ya kwanza kutwajwa kwa kesi hii kortini.

 

error: Content is protected !!