Marufuku kuvua kondomu wakati wa kujamiiana

HomeElimu

Marufuku kuvua kondomu wakati wa kujamiiana

Baada ya miaka 4, Jimbo la California nchini Marekani limepitisha sheria mbili ambazo zinalenga kudhibiti makosa ya kingono ambapo sheria ya kwanza imefanya kuwa kosa kwa mshirika mmoja kuvua kondomu bila ridhaa ya mwenzake wakati wa kujamiina.

Sheria hii iliwasilishwa kwenye bunge la jimbo hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2017 na Cristina Garcia, na sasa inatoa fursa kwa mwathirika wa kitendo hicho kufungua kesi na kudai fidia.

Lengo kuu la sheria hiyo ni kudhibiti usambazaji wa magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa zinazotokana na kutotumia kondomu wakati wa kujamiiana.

Aidha, sheria ya pili imefanya kuwa kosa kwa mwanandoa mmoja kumlazimisha mwanandoa mwenzake kufanya tendo la ndoa, kitendo ambacho sasa kitatambulika kama ubakaji. Msingi wake ni kwamba tendo hilo linapaswa kuridhiwa na washirika wote wawili.

Sheria hii imetokana na maboresho ya sheria ya ubakiaji iliyokuwepo awali ambayo haikuwa ikitambua kwamba kunaweza kutokea ubakaji ndani ya ndoa.

 

error: Content is protected !!