Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inavyoitekeleza kauli ya Kazi Iendelee, ndani ya miezi 20 Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kuibadilisha Tanzania huku matunda ya utendaji kazi wake yakionekana kupitia sekta mbalimbali.
Uchumi– Ukusanyaji wa mapato umeongezeka kwa wastani wa sh trilioni 1.74 kwa mwezi kwa mwaka 2021/22 ikilinganishwa na sh trilioni 1.46 kwa mwaka 2020/21.
Sekta ya utalii– Kutokana na mazingira wezeshi na kusimamia mikakati ya kukuza vivutio vya utalii, idadi ya watalii wa nje imeongezeka kutoka watalii 620,867 mwaka 2020 hadi 922,692 mwaka 2021 sawa na ongezeko la 32.7%.
Sekta ya afya– Ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya kuanzia zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na hospitali za rufaa.
Sekta ya elimu– Serikali inaendelea kutoa elimu bila ada katika ngazi za shule za awali, msingi, sekondari huku ikitoa ufadhili pamoja na mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Sekta ya maji– Upatikanaji wa maji safi na salama mjini imeongezeka kutoka 84% mwaka 2020 hadi 86% mwaka 2022 na vijijini kutoka 70.1% mwaka 2020 hadi 74.5% mwaka 2022.
Sekta ya nishati– Mikakati madhubuti imewekwa na serikali kuimarisha sekya ya nishati ili kuongeza uzalishaji wa umeme kwa vyanzo mbalimbali ikiwamo ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme megawati 2,115 wa Julius Nyerere ambao umefikia 77.15%.
Ushirikiano wa Kimataifa– Serikali imeendela kuimarisha mashirikiano ya kikanda katika kuboresha mahusiano na kukuza diplomasia ya siasa ya uchumi.