Mjue Mtanzania aliyehusika kufichua Skendo ya Pandora

HomeKimataifa

Mjue Mtanzania aliyehusika kufichua Skendo ya Pandora

Pandora ni skendo inayohusisha watu mashuhuri duniani na mtandao mkubwa wa shughuli haramu katika masuala ya fedha na uwekezaji. Skendo hii inahusisha viongozi wa ngazi za juu hasa Marais toka mataifa mbalimbali duniani walioko madarakani na waliostaafu. Pia kuna Mawaziri Wakuu, Majaji na baadhi ya familia tajiri za kifalme duniani.

Uvishaji wa taarifa hizi za siri umetekelezwa na waandishi wa habari 600 kutoka nchi 177 duniani ambapo wamekuwa wakipekua nyakara zaidi milioni 11 ambazo zinabeba taarifa nyeti za watu mashuhuri. Kwenye jopo hilo la wanahabari ambao chama chao kinaitwa ICIJ chenye makao yake makuu Washington nchini Marekani, yumo Mtanzania ambaye amehusika kufichua ghiliba zinayofanywa na viongozi wakubwa kwenye umiliki wa miradi mbalimbali ya uwekezaji.

Ni nani huyo?
Jina lake ni Simon Mkina, ameshinda tuzo kadhaa hasa za kwenye uandishi wa habari za uchunguzi. Ni mhariri na pia mkufunzi katika masuala ya habari na pia amechapisha machapisho kadhaa zenye tasnia ya habari ndani ya miaka 26 ya uzoefu wake kwenye habari.

                                   > Pandora Leaks: Tambua njia wanazotumia viongozi wakubwa duniani kuiba mali

Amefanya kazi na vituo vya habari vingi na vikubwa ndani na nje ya nchi, kama vile Uhuru, Mzalendo, Kulikoni, This Day, HabariLeo, Daily News, Zanzibar Leo na Mawio.

Simon ni mwandishi huru anayefanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi au mikataba isiyofungamana na muda na eneo la kazi (freelancer) kwa mashirika makubwa ya habari likiwemo la ICIJ, The Continent pamoja na Mail & Guardian.

Katika kazi yake amewahi kufichua skendo nyingi za rushwa na pia ni mwanaharakati wa mambo ya utawala bora. Kwa sasa ni Rais wa chama kinachoitwa “Tanzania Media Practitioners Association”

error: Content is protected !!