Mtambo wa kusaidia watu kujiua waanza kutumika

HomeKimataifa

Mtambo wa kusaidia watu kujiua waanza kutumika

Uswizi wamepitisha uamuzi wa watu kutumia mashine ambayo itawasiadia kujiua bila mateso lakini pia itasaidia mtu kuamua ni wapi na saa ngapi anataka kujiua.

Bodi ya madawa ya nchi hiyo ilipitisha mtambo wa kujiua wa ‘Sarco’ ambao mtu huingia ndani ya mtambo huo na kuanza kuuendesha na atakapokufa mtambo huo utatumika kama jeneza lake.

Mgunduzi wa mtambo huo Philip Nitschke, amesema kwa sasa watu wanaojiua nchini humo wanatumia vidonge pamoja na mchanganyiko ambao unaweza kumfanya mtu apoteze fahamu na kupata maumivu kabla ya kufariki.

Lakini sasa kwa kutumia mtambo huo, mtu anaweza kuingia ndani ya mtambo na kuanza kujibu maswali ambayo yalirekodiwa kabla na akimaliza atabonyeza kitufe kinachoruhusu hewa ya Nitrojeni kuingia ndani,jambo litakalopelekea kupungua kiwango cha hewa ya Oksijeni iliyopo ndani ya mtambo huo kutoka nyuzi 21 mpaka nyuzi 1.

Mgunduzi huyo anasema mtambo huo una faida kubwa kwani haumsababaishii mtu anayetaka kujiua maumivu makubwa, wala hauitaji ruhusa ya mtu yoyote kutekeleza tukio hilo. Wakati wa kujiua kwa msaada wa mtambo huo mtu anaweza akahisi kama kuchanganyikiwa kidogo kabla hajafariki.

Kwa baadhi ya nchi pia kama Ujerumani, Ubelgiji na Canada inakubalika kisheria kumsaidia mtu kujiua, huku nchini Canada zaidi ya watu 7,600 walisaidiwa kujiua mwaka jana.

error: Content is protected !!