Mvua 30 kwa kunajisi mtoto wa dada yake

HomeKitaifa

Mvua 30 kwa kunajisi mtoto wa dada yake

Mahakama ya Wilaya ya Tarime imemuhukumu mkazi wa kijiji cha Rebucheri, Tarime mkoani Mara, Mandashi Marwa (23) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mtoto wa dada yake.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Yohana Myomba alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri, mahakama imeridhika pasina shaka lolote, hivyo kumtia hatiani mshtakiwa chini ya kifungu cha 130(1) na 131 cha 3 kanuni ya Adhabu Sura ya 16 mapitio ya 2019.

“Nakuhukumu kwenda jela miaka 30 ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia mbaya kama wewe, wanaoharibu maisha ya watoto wa watu wengine. Kama hukuridhika na adhabu hii rufaa iko wazi,” alisema Hakimu Myombo.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa polisi, Bugombe Bukuru, mshtakiwa alimfanyia mtoto huyo kitendo hicho kwa nyakati tofauti usiku kati ya Juni na Agosti, 2021. Bukuru alidai kuwa mama wa mtoto huyo aligundua mtoto wake kufanyiwa kitendo hicho na kuumizwa vibaya huku akishindwa kutembea.

error: Content is protected !!