Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amesema Watanzania wanapaswa kukubaliana kwanza kuhusu umuhimu wa kuzungumza juu ya mchakato wa Katiba kabla ya kuweka shinikizo kubwa kwa viongozi.
Akizungumza leo mkoani Dodoma wakati akishiriki maadhimisho ya Siku ya Vijana yaliyoandaliwa na Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), Mwabukusi amesema shinikizo kubwa linaweza kuwakatisha tamaa viongozi au kuwafanya washindwe kuzungumza kuhusu mchakato huo.
Amesema ni muhimu kuweka mazingira yanayowezesha mazungumzo kuhusu Katiba kufanyika kwa utulivu na ushirikishwaji, badala ya kutumia shinikizo linaloweza kuzuia viongozi kushiriki katika mchakato huo.


