Rais Samia asema urithi bora kwa watoto ni taifa lenye amani

HomeKitaifa

Rais Samia asema urithi bora kwa watoto ni taifa lenye amani

Rais Samia Suluhu Hassan amesema urithi mkubwa ambao wazazi na walezi wanapaswa kuwaachia watoto wao ni taifa lenye amani ambalo wataweza kutimiza ndoto zao.

Amesema hayo wakati akizindua kiwanja cha michezo ya watoto cha Kizimkazi, Zanzibar ambacho kina uwezo wa kuhudumia zaidi ya watoto 500 kwa wakati mmoja kupitia shughuli mbalimbali zinazolenga kujifunza, burudani, kukuza vipaji na ustawi wa watoto.

“Nitoe rai kwa wazazi na walezi wenzangu kuendelea kuwalea watoto wetu katika misingi ya maadili na nidhamu, upendo na amani. Urithi wa maana tunaoweza kuwaachia si mali peke yake, bali taifa salama lenye amani ambalo wataweza kutimiza ndoto zao,” amesema Rais Samia Suluhu.

Aidha, Rais Samia amesema kupitia michezo watoto hujifunza tabia njema, ubunifu, nidhamu, heshima na ushirikiano ambavyo ni vichocheo muhimu katika kujenga utu, maadili, uwezo wa kuchangamana na wengine na kukua kiakili.

error: Content is protected !!